Wakati mtandao wa instagram ukisherehea kutimiza watumiaji Bilioni 1 duniani kote, wamiliki wameonekana kuongeza nguvu na kuwa wabunifu zaidi katika mtandao huo kwa kubuni vitu tofauti tofauti kuboresha huduma zao.
Instagram leo June 20 2018 wametangaza kuanzisha IGTV ambayo ni app itakoyokuwa inapatikana katika simu za android na IOS, kwa ajili ya watumiaji wa mtandao wa instagram kupost video zenye urefu wa kuanzia wa dakika 10 hadi saa moja kwa watumiaji wenye wafuasi wengi kwa kuanzia lakini baadae ni wote watakuwa na uwezo wa kupost video ya saa moja.
IGTV baada ya kuzinduliwa na kuelezewa sifa zake mbalimbali imeanza kufananishwa kama ni mshindani mpya wa mtandao wa YouTube kwani kwa sasa IGTV haitakuwa inawalipa watengeneza maudhui lakini kwa siku za usoni itakuwa inawalipa kama ambavyo YouTube wanafanya kwa sasa.
IGTV video zake zitakuwa wima kama zilivyo za instalive kwa sasa, app inajitegemea lakini kwa walioyo na app ya instagram watakuwa na uwezo wa kupata huduma ya IGTV kupitia instagram account zao za kawaida, IGTV unaweza kupost video kwa simu au computer.
FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018