Leo June 22,2018 tunayo story kutoka kwa Kaimu Mkurugemzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi, Godfrey Mbanyi ambapo ametangaza matokeo ya mitihani ya Wataalamu wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi, huku akisema kuna ongezeko la ufaulu.
Mbanyi amesema katika matokeo hayo ufaulu umeongezeka hadi kufikia asilimia 56 ikiwa ni tofauti na matokeo ya mwaka 2017 ya asilimia 48,
“Mbali na matokeo haya pia kuna tatizo la ufaulu hafifu hasa katika mitihani ya Hesabu, lakini tutahakikisha tunaweka mikakati ili watu wasiigope, “amesema Mbanyi