Leo June 22, 2018 Shirika moja la Umma nchini Japan limewaomba msamaha Raia wa Japan kutokana na Mfanyakazi wake mmoja kwenda mapumziko ya chakula cha mchana dakika tatu kabla ya muda uliopangwa.
Mfanyakazi huyo mwenye miaka 64 ametajwa kuwa na tabia hiyo ya kwenda kula chakula cha mchana kabla ya muda stahili uliopangwa.
Kwa mujibu wa taratibu za shirika hilo Mfanyakazi anatakiwa aende mapumziko ya chakula cha mchana saa 6 mchana na kurudi ofisini saa 7 mchana lakini mfanyakazi huyo aliwahi kutoka ofisini kwake kabla ya saa 6 mchana kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wa Shirika hilo.
Aidha Shirika hilo limempiga faini Mfanyakazi huyo na kumpa adhabu kali kwa kosa hilo. Na Kwa kuongezea tu nchi ya Japan inatajwa kwa kuzingatia sana muda wa kazi.