Leo June 22, 2018 Idadi ya viongozi wakuu wanawake ambao wamejifungua wakiwa madaraka imefikia wawili mara baada ya waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Arden kupata mtoto wa kike jana.
Mwingine kujifungua madarakani ni waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto, aliyejifungua mtoto wa kike mnamo mwaka 1990. Alikuwa kiongozi wa kwanza kujifungua akiwa ofisini.
Hii inamfanya Jacinda awe kiongozi wa pili katika historia aliye madarakani kujifungua mtoto.
Jacinda alilazwa kwenye hospitali moja mjini Auckland siku ya alhamisi.
Mbali na kuwa Kiongozi wa pili katika historia kujifungua akiwa uongozini, ni waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi kuliongoza taifa la New Zealand tangu 1856.
Akiwa na umri wa miaka 37 atachukua mapumziko kwa muda wa wiki sita huku Naibu wake, Winston Peters akichukua usukani.
Hata hivyo ushauri wake utahitajika kwa baadhi ya masuala muhimu ikiwemo kusoma kumbukumbu ya mkutano wa mawaziri licha ya kuwa likizoni.
“Niko na hakika tunapitia hisia nyingi zinazopitiwa na wazazi wengine pia, na vile vile tunatoa shukrani kwa ukarimu na taarifa za pongezi kutoka watu wengi. Asanteni.” Aliongeza kwenye taarifa aliyotoa.
Mbowe asababisha kesi ya Viongozi 8 wa CHADEMA kuahirishwa