Taarifa mpya ya kuifahamu leo June 23, 2018 ni kumhusu Rais wa Marekani Donald Trump ambapo ameidhinisha upya vikwazo dhidi ya Korea kaskazini akitaja taifa hilo kuwa ’tishio liliso la kawaida’ kutokana na silaha zake za nyuklia ikiwa ni siku 10 tu baada ya kutamka kwamba hakuna hatari yoyote kutoka kwa Pyongyang.
“Hakuna tena tishio kutoka Korea kaskazini,” alisema maneno hayo June 13, siku moja baada ya kukutana na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un huko Singapore.
Hatua hiyo imekuja wakati Marekani na Korea kusini zimefutilia mbali mazoezi mawili ya pamoja ya kijeshi.
Wizara ya ulinzi Marekani Pentagon imesema lengo ni kuunga mkono majadiliano ya kidiplomasia.