Leo June 23, 2018 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua mifumo tisa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dodoma.
Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Mkuu ameagiza mifumo ya utoaji huduma Serikalini kwa njia ya mitandao isitumike kukwamisha shughuli za Serikali au Mipango ya utoaji huduma kwa wananchi.
Mifumo hiyo aliyoizundua inahusu utoaji Huduma Serikalini ambayo ni Mfumo wa Usajili wa Vizazi na Vifo, Mfumo wa Taarifa za Kitabibu, Mfumo wa Taarifa za Ununuzi, Mfumo wa Kumbukumbu za Kielektroniki na Mfumo wa Ofisi Mtandao.