Beki wa zamani wa Barcelona na Uhispania Carles Puyol amepigwa marufuku kushiriki katika kutangaza kipindi cha kombe la dunia nchini Iran kwa kuwa na nywele ndefu.
Licha ya kukubali kushiriki kwenye kipindi cha kutangaza mechi ya kombe la dunia kati ya Uhispania na Iran na hata kuwasili Iran, Puyol alilazimika kubaki kwenye hoteli baada ya kunyimwa ruhusa kutangaza mchuano huo.
Puyol alitarajiwa kushiriki kipindi hicho special kwenye kituo cha IRTV 3 akiwa na mtangazaji Adel Ferdosipour.
Puyol alifahamishwa na idhaa ya taifa ya IRIB hangeweza kushiriki kwenye kipindi kwani nywele zake zilikuwa ndefu na kukinzana na mafunzo ya Kiislamu.
MAGAZETI LIVE: Maandamano ya ‘BWEGE’ yakutanisha wabunge, Baadhi ya vigogo CCM wezi’