Mbunge wa Mtwara vijijini Hawa Ghasia zipo taarifa zinazodai kwamba kuna njama zimeundwa na baadhi ya Wabunge wenzao ili kuweza kuwadhalilisha wale wote wanaotetea maslai ya wakulima wa zao la korosho nchini.
“Kwa masikitiko makubwa sana ambayo yanasambazwa kwa makusudi dhidi ya Wabunge wanaotetea kupelekewa pembejeo kwenye maeneo yao, tuna taarifa watu wamekaa vikao ili waje huku kutudhalilisha tunaotetea wananchi wetu kupewa pembejeo za korosho” –Hawa Ghasia
“Napenda niwahakikishe wananchi wanaolima korosho kwamba Wabunge wao tupo imara tutapambana kuhakikisha haki zao zinapatikana na hata zisipopatikana wajibu wetu tutautimiza kama wawakilishi wa wananchi kuja kuwatetea” –Hawa Ghasia
MAHAKAMANI: Sababu kesi ya Mbowe kukwama kusikilizwa