June 26, 2018 Waziri wa Fedha na mipango Dr Philip Mpango wakati akijibu hoja za Wabunge kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 amesema kuwa hana lengo la kuwakomoa wakulima wa zao la korosho kama baadhi ya Wabunge wanavyotuhumu.
“Ni vyema niseme na watanzania wasikie, mimi siwezi kamwe kuwahujumu wakulima wa korosho wa Mtwara na Lindi au mkoa mwingine wowote ule na niwahakikishie nitakwenda Mtwara na Lindi na hakuwa wakunizuia ni haki yangu na uhuru wangu kama Mtanzania ambayo haiwezi kupokonywa kwa vitisho na hata ikibidi kufa na iwe” –Dr Philip Mpango
“Kuna Wabunge wameandaliwa waje kutudhalilisha, Mungu atawaumbua” -Hawa Ghasia