Ikiwa yamesalia saa kadhaa ili Wabunge wapitishe makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 kwa kupigiwa kura za NDIO au HAPANA Spika Job Ndugai alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha Wabunge wake kuhusu kanuni zilizopo ikiwemo Rais kulazimika kulivunja Bunge endapo bajeti hiyo haitapitishwa.
“Mjadala kuhusu bajeti ya Serikali utaitimishwa na Waziri wa Fedha baada ya hapo Bunge litapiga kura ya wazi leo jioni kwa kuita jina la Mbunge mmoja mmoja, endapo mlio wengi mkiikataa bajeti Rais atalazimika kulivunja Bunge mara moja na baadhi ya wengine mkirudishwa jimboni hamrudi hapa” –Spika Job Ndugai
“Sitayumba hata ikibidi kufa na iwe” –Waziri Mpango