June 26, 2018 nakusogezea taarifa ya uzinduzi wa programu ya miezi mitatu na shindano ambalo linalengo la kuwaongezea uwezo wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia stadi za biashara, ufahamu na kisha kuwapatia zaidi ya Millioni 10 kwa wazo bora la biashara litakalokuwa limewasilishwa.
Shindano linalojulikana kama ‘Kuza Ofisi na finca’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya 4 za mkoa wa DSM, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.
Akiongea wakati wa uzinduzi jijini DSM, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Finca, Nicholous John amesema lengo ni kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao, Mshindi wa programu na shindano hili atawezeshwa kifedha kuendeleza biashara zake ndogo ndogo ziliyopo.
“Shindano hili litashirikisha wateja wa Finca wenye akaunti na wale ambao wanapenda kushiriki watatakiwa kufungua akaunti ya Finca, ambao pia watatakiwa kuweka kiasi cha TZS 20,000 watatakiwa kujaza fomu ambapo watabainisha katika fomu hizo kuwa wataenda kufanyia nini zawadi hiyo katika biashara zao iwapo wataibuka kuwa washindi.” -John
“Baada ya hapo fomu hizo zitawasilishwa katika matawi yetu, mpaka hapo watakuwa wametimiza vigezo vya hatua ya kwanza ya shindano”.
“Mwishoni mwa shindano, mshindi mmoja mwenye bahati ataondoka na zawadi nono ya zaidi ya TZS milioni 10″, Alisema Nicholous, akiongeza kwamba washiriki wengine wenye vigezo pia watakuwa na nafasi ya kujipatia mikopo kutoka benki hiyo.” amesema John
Naye Afisa Mkuu wa Biashara wa benki ya Finca, Emmanuel Zambi amesema: “Kampeni ya Kuza Ofisi na FINCA ni sehemu ya FINCA kusherehekea miaka 20 ya uendeshaji wa shughuli zake nchini Tanzania ambapo benki ya FINCA imekuwa maarufu kwa utoaji wa masuluisho bora na aina mbalimbali za akaunti, Mikopo na huduma zingine ambazo zinajumuisha mahitaji ya watu binafsi na taasisi.”
King Majuto “Zipo Kampuni nimefanya kazi, mikataba ninayo wamekimbia na hela zangu”