Leo June 27, 2018 India imetajwa kuwa taifa hatari zaidi duniani kwa usalama wa wanawake, kutokana na unyanyasaji wa kingono na kushurutishwa kuingia kwenye kazi za utumwa, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mfuko wa Thomas Reuters uliohusisha wataalamu 550 wa masuala ya wanawake.
Afghanistan na Syria zimeorodheshwa kuwa za pili na tatu huku Somalia, Congo na Saudi arabia zikifuata.
Data za serikali zinaonyesha kuwa ripoti za uhalifu dhidi ya wanawake zimepanda kwa asilimia 83 kati ya mwaka 2007 na 2016, ambapo kulikuwa na kesi nne za ubakaji zilizokuwa zikiripotiwa kila baada ya saa moja.