Leo June 28,2018 tunayo good news kuhusu wakulima wa zao la muhogo nchini baada ya kuzinduliwa kwa kiwanda cha uchakataji Mihogo cha Kanton mkoani Tanga ambapo itasafirishwa kwenda nchini China.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amewataka wakulima wa wilaya hiyo kuongeza uzalishaji wa Mihogo kwa sababu ni zao lenye faida.
Gondwe amesema kuwa endapo kama zao hilo litapewa kipaumbele litaibua fursa nyingi ikiwemo kubadilisha maisha ya wakulima.
Mwakilishi wa kampuni ya Kanton, John Rwehumbiza amesema Kampuni hiyo imefanya uwekezaji wa Dola Mil 10, ambapo wanatarajia kuwaajiri watu 100 na kuchakata tani 200.
“Kiwanda hiki ni cha teknolojia hivyo tunaongea na serikali ili tápate maeneo yetu kama shamba darasa ili kuhakikisha kiwanda? hakiwezi kusimama,” amesema Rwehumbiza