Leo June 27,2018 tunayo Exclusive story kutokea kwa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Afya na Akili, Profesa Sylvia Kaaya ambaye ameshinda tuzo ya Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa Magonjwa ya Akili kutokea nchini Marekani.
Prof. Kaaya ambaye anatokea Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), ameshinda tuzo hiyo wiki chache zilizopita.
Katika exclusive na AyoTV na millardayo.com, Prof Kaaya amesema tuzo hiyo ya heshima imetolewa na Chuo Kikuu cha Dartmouth.
“Kwa kweli ni bahati maana ukiniuliza ilikuaje nimeshirikishwa na nimeshinda nitakwambia sijui, lakini kuna vigezo mbalimbali walinambia wameviangalia ikiwemo jitihada ninazozifanya kuhusu afya ya magonjwa ya akili,” amesema Prof. Kaaya
Pia amesema kuwa katika tuzo hiyo ilishirikisha Madaktari bingwa 6, watano wakitokea Marekani na kwa Bara la Afrika alikuwa peke yake akitokea nchini Tanzania.
“Naweza kusema hii ni tuzo ya wote kwa sababu katika tafiti tunazozifanya ninashirikiana na wenzangu,” Kaaya
Zinaitwa ‘Powerbank’ Arusha, ‘busta’ Dar zazua mjadala, muuzaji anapata elfu 70