Uwekezaji huo umetajwa kugharimu dola Milioni 20, ambao utengeneza ajira 1,000. Katika uzinduzi wa tukio hilo Rais Paul Kagame, amesema kuwa ni hatua muhimu kwa nchi hiyo.
Amesema kuwa bila shaka kituo kinawakilisha sura mpya katika safari ya mabadiliko ya kiuchumi Rwanda.
“Najua kwa wengine inaweza kuwa vigumu kuamini kuwa magari ya Ujerumani, kama tulivyozoea kuwaita, yangeundwa kweli nchini Rwanda.” Kagame.
Hata hivyo bado umiliki wa magari nchini Rwanda bado ni mdogo ambapo kati ya watu milioni 12, laki mbili tu ndiyo wanaotumia magari binafsi hao ni wale waliosajiliwa tangu mwaka 1997 kwa mujibu wa mamlaka ya ukusanyaji wa kodi.
Licha ya kiwango cha chini cha umiliki wa magari nchini Rwanda, Volkswagen inatarajia kuuza magari hayo nchi za jirani za jirani huku mengine yakitarajiwa kutumika katika biashara ya usafiri ya kimataifa kimataifa kama vile ‘Uber’ ambapo itawezesha watu kuagiza safari kupitia simu za kisasa
LIVE MAGAZETI: Dude la Korosho Kung’oa mtu, hoja za wabunge zaipa tabu serikali