Mahakama nchini Sudan imetengua adhabu ya kifo kwa msichana Noura Hussein, ambaye alimuua mumewe baada ya mwanaume huyo kumbaka, katika kesi ambayo imeweka wazi juu ya ndoa za kulazimisha kwa watoto na ubakaji ndani ya ndoa katika taifa hilo la Afrika.
Timu ya wanasheria waliliambia shirika la utangazaji la CNN Jumanne kwamba, Noura, mwenye umri wa miaka 19 sasa, amepewa adhabu ya miaka mitano jela kwa kumuua mwanaume wa miaka 35.
Mahakama pia imetoa amri kwa familia yake kulipa paundi 337,000 za Sudan (sawa na 42,075,000 za Kitanzania) kwa familia ya wafiwa.
Wanasheria wake wanasema wanapanga kukata rufaa kwa kifungo na pia malipo.
King Majuto “Zipo Kampuni nimefanya kazi, mikataba ninayo wamekimbia na hela zangu”