Leo June 28,2018 nakuletea stori kutoka huko nchini Urusi ambapo unaambiwa kuwa FIFA inamlipa Diego Maradona zaidi ya Milioni 29 za Kitanzania na kumgharamia gharama zingine za chakula, malazi na usafiri gwiji huyo wa soka duniani ili aweze tu kwenda kutazama mechi za Kombe la Dunia nchini Urusi.
Rais wa FIFA ndie aliyekuja na wazo hilo la kuhakikisha waliokuwa magwiji wa kusakata kabumbu wanahudhuria michuano hiyo ya Kombe la Dunia ikiwa na lengo la kuwapa heshima magwiji hao na kuwavutia mashabiki wengine kwenda uwanjani kutazama michuano hiyo.
Kwa upande mwingine wakosoaji wamekuwa wakiishutumu FIFA kuwa walikosea kumchagua Maradona katika nafasi aliyopewa kutokana na kuonekana akionesha ishara za matusi wakati alipokuwa akiishabikia timu yake ya Argentina dhidi ya Nigeria na kuonekana kuwa anaichafua FIFA.
Rais Magufuli alivyompokea Rais wa Zimbabwe Mnangagwa