Leo June 28, 2018 Mkuu wa wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, Rehema Madusa amesema kuwa kuna baadhi ya wakemia wilayani humo ambao si waaminifu na wanatumia vibaya taaluma yao kwa kuwaibia wananchi dhahabu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya matumizi ya kemikali kwenye madini, amesema kuwa mbali na kuwanyima haki yao wananchi, wakemia hao pia wamekuwa wakiikosesha serikali mapato.
Mkurugenzi wa idara ya usimamizi na udhibiti kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Christopher Nyambo amesema kuwa kwa mujibu wa sheria kila mtu anayejihusisha na matumzi au usambazaji wa kemikali anapaswa kusajiliwa na kupata mafunzo maalum.
Aliwataka watumiaji wote wa kemikali kujisajili na kuwa waaminifu ili kuepusha athari za kiafya na mazingira zitokanazo na matumizi yake.
Rais Magufuli alivyompokea Rais wa Zimbabwe Mnangagwa