Alhamisi ya June 28 2018 bara la Afrika lilikuwa na imani kuwa timu ya taifa ya Senegal ndio litakuwa taifa pekee la Afrika kuingia hatua ya 16 bora ya michuano ya World Cup 2018, hiyo ni baada ya kuingia uwanjani kupambana dhidi ya Colombia ikiwa inahitaji point moja.
Senegal ilihitaji walau point moja na kuendelea ili ipate nafasi ya kucheza hatua ya 16 bora, hivyo Colombia kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Yerry Mina dakika ya 74, linawafanya Senegal kuaga michuano hiyo licha ya kufanana kila kitu na Japan waliofanikiwa kuingia hatua ya 16 bora.
Japan anafuzu kwa kipengele cha fair play yaani Japan wameoneshwa kadi chache za njano zaidi ya Senegal waliofanana nao kila kitu, hivyo sasa ni wazi Afrika haina muwakilishi hata mmoja katika hatua ya 16 bora, timu zote 5 zilizokuwa zinaiwakilisha Afrika zimetolewa katika hatua ya makundi.
Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake