Leo June 28,2018 tunayo story kutoka kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo kimezungumzia afya ya Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya CHADEMA, Tumaini Makene amesema Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki anaendelea vizuri na afya yake inazidi kuimarika.
“Amemaliza kufanyiwa upasuaji wa 20 na anaendelea na mazoezi ya awali, anatamani kurudi Tanzania ili kuendelea kuzungumzia mambo yanayohusu nchi akiwa hapa,” amesema Makene