Leo June 28, 2018 Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu amezindua msimu wa ukusanyaji na ukoboaji wa Kahawa mkoani Kagera kwa mwaka 2018/2019 huku akisema kuwa serikali imeagiza kahawa kuuzwa katika vyama vya ushirika na si kiholela.
Meja Jen. Kijuu amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanaendelea kufanya biashara hiyo kimagendo huku wengine wakinunua kahawa kiholela na kuwataka kuacha biashara hiyo mara moja kwani kuanzia leo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
“Vyama vya ushirika ndio pekee watakusanya Kahawa za wakulima na kuhakikisha zinapata soko zuri kwa usimamizi wa Serikali, najua wenye nia mbaya wanaendelea kujihusisha na magendo ya kahawa suala hilo likome, tukikukamata tutataifisha” Meja Jen. Kijuu
EXCLUSIVE: CHADEMA waweka wazi atakachozungumza Lissu akiingia Tanzania