Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya England Wayne Rooney Alhamisi ya June 28 2018 amewasili rasmi katika club yake mpya ya DC United inayoshiriki Ligi Kuu Marekani MLS.
Rooney amewasili DC United akitokea Everton ya England na kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu na ataanza kutambulika kama mchezaji rasmi wa DC United, dirusha la usajili litakapofunguliwa July 10 2018.
Wayne Rooney ambaye amewahi kuwa nahodha wa Man United na timu ya taifa ya England, amewasili Airport akiwa DC na kupokelewa na mamia ya mashabiki ambao wamefuraishwa na ujio wake katika club yao.
Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake