Leo June 29, 2018 Watu watano wameuawa kwa kupigwa risasi katika majengo ya gazeti la Capital Gazette huko Maryland, nchini Marekani. Mtuhumiwa anahojiwa na polisi wa Kaunti.
Kwa mujibu wa Sun Baltimore, mmiliki wa Capital Gazette tukio hilo lilitokea saa 2:40 usiku. Watu watano wameuawa na wengine wawili waejeruhiwa, kulingana na ripoti iliyotolewa na Bill Krampf, kaimu Mkuu wa polisi, mbele ya waandishi wa habari. Tukio hilo ni “shambulizi lililolenga gazeti la Capital Gazette,” Bill Krampf amesema, akiongeza kuwa gazeti hilo limekua likipokea vitisho kwenye mitandao ya kijamii.
Mtuhumiwa amekamatwa na anahojiwa na polisi, amesema Steven R. Schuh, kiongozi wa Jimbo la Anne Arundel. Wafanyakazi wa gazeti hilo wanasema mshambuliaji huyo ambaye ni mzungu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 ambaye alijiharibu vidole vyake ili kuepusha kutambulika kwa alama za vidole alifyatua risasi hovyo kupitia mlango wa vioo.
Kupitia mtandao wa twiter wanahabari kadhaa waliokuwa katika ofisi hiyo akiwemo Jimmy DeButts ambaye ni mhariri mkuu katika kampuni ya Capital Gazette wameelezea masikitiko yao kufuatia vifo vya wenzao huku wengine wakisema kwamba walikuwa ni kama ndugu zao.
Ikulu ya White House imesema kuwa rais wa Marekani Donald Trump amearifiwa kuhusu hali hiyo huko Annapolis. “Naziombea familia zilizopoteza ndugu zao pamoja na wote waliopatwa na janga hilo,” Donald trump ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter.
MAGAZETI LIVE: Biashara ya kushikwa nyeti, matiti yaibuka, Mateso ya korosho