Leo June 30,2018 tunayo story kuhusu wauzaji wa nyama ambapo kwa mujibu wa sheria mtu hapaswi kuchinja nyama bila kibali maalum.
Wakili wa kujitegemea Leornad Manyama anasema kuwa endapo mtu akitenda kosa la kuuzia watu nyama wasiyoitaka ni kifungo jela kisichozidi miezi 6 ama faini isiyozidi Sh.Milioni 1.
“Hata kama utachinja mbuzi ama mnyama kwa ajili ya matumizi binafsi ya nyumbani kama sherehe lazima athibitishwe kwa kupewa kibali na Mamlaka ya Chakula Tanzania TFDA,” amesema Manyama
Pia amesema sheria hizo zipo ili kulinda afya ya walaji wa nyama na sio kuwakomoa.