Leo July 2,2018 tunayo story kutokea kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo limebainisha kuwa litahakikisha kila Mtanzania anapata nyumba kulingana na kipato chake.
Meneja Mauzo wa NHC, Stephen Mema Afisa amesema kuwa mahitaji ya nyumba ni makubwa kwa sasa ikilinganishwa na awali. “Ni malengo yetu kuhakikisha kila Mtanzania anapata nyumba na zinaendana na kile kipato chake,”
Pia amebainisha kuwa kwa sasa wamekuwa na utofauti ikilinganishwa na maadhimisho ya sikukuu ya Saba Saba yaliyopita ambapo wameongeza idadi ya miradi.
Amesema kuwa miongoni mwa miradi na maeneo yenye uhitaji wa nyumba ni Dodoma kwa sababu serikali inahamia huku, ambapo tayari wamemaliza hatua ya kwanza maeneo ya Iyumbu Dodoma.
LIVE MAGAZETI: Madude yaliomng’oa Mwigulu, Watu 20 wafa kwa ajali Mbeya