Leo July 2, 2018 kuna hii ya kuifahamu kutoa kwa Mfalme Mswati wa swaziland ametuma mswaada bungeni akitaka kutungwa kwa sheria mpya kwa raia kutoka nje ya nchi hiyo kulipa kodi watakapofunga ndoa na wanawake nchini Swaziland kwa kutozwa kiasi cha dola 2,200.
“ Lengo la sheria hii ni kuwalinda wanawake na matendo ya unyanyasaji kutoka kwa wapenzi wao wa kigeni wanaotumia njia ya kuoa wanawake wetu kwa ajili ya kupata uraia” Msemaji wa Serikali Percy Simelane.
Aidha mswada huo umepingwa vikali na mmoja wa wanaharakati wa kutetea haki za wanawake Dumsane Dlamini akidai kuwa sheria hiyo itawanyima haki wanawawake nchini Swaziland maana wanawake hao huwapenda wanaume wa kigeni kwa utanashati na wanajua thamani ya mapenzi.
Lakini 2016, Wizara ya mambo ya Kigeni ilianzisha mpango wa kutoa uraia kwa wageni nusu milioni hasa kutoka Asia ambao watakuwa sehemu ya idadi ya raia 1.3 milioni ya wananchi wote wa Swaziland .