Leo July 3,2018 nakusogezea stori kutoka huko nchini Iran ambapo unaambiwa kuwa Kiongozi mkuu wa idara ya ulinzi nchini Iran Brigadier General Gholam Reza Jalali ameishutumu nchi ya Israel kuiba mawingu ya mvua ya nchi yake na kuisababisha nchi hiyo kukumbwa na ukame.
Kiongozi huyo ameyaeleza hayo alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari na kuongeza kuwa nchi ya Israel imekuwa ikiwahujumu kwa kuharibu mawingu ya mvua ya nchi yao katika anga lao na kuwasababishia ukame.
Aidha Kiongozi huyo katika utetezi wa shutuma zake hizo kwa nchi ya Israel ameeleza kuwa milima yote ya Afghanstan na ile ya Mediterranean ina theluji kasoro milima yao kitu anachosema kuwa ni hujuma za taifa la Israel.
Kwa muda mrefu mahusiano kati ya mataifa ya Israel na Iran yamekuwa na utata na shutuma hizi ni kama zinatia chumvi kidonda cha mahusiano ya mataifa hayo mawili.