Shirikisho la soka Tanzania TFF leo kupitia kwa kaimu katibu mkuu wake Kidao Wilfred limetegua kitendawili kilichokuwa kinaulizwa na wengi baada ya club ya Mtibwa Sugar kutwaa Ubingwa wa Kombe la FA kwa kuifunga Singida United.
Kwa kawaida mshindi au Bingwa wa Kombe la FA ndio huwa anapewa nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika, sasa baada ya ushindi huo wengi walitaka kufahamu kuwa Mtibwa ambaye alifungiwa na CAF kushiriki michuano hiyo kwa kosa la kutokwenda South Africa kucheza game ya marudiano dhidi ya Santos FC hatma yake ipoje.
TFF ambaye imepatiwa majibu na CAF kuwa ili Mtibwa Sugar ipate nafasi ya kushiriki michuano hiyo inatakiwa kulipa faini ya dola 1500 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni tatu na gharama zote za Santos za kuja Tanzania kwa ajili ya game hiyo, pesa hiyo inatakiwa kulipwa hadi kufikia July 20 2018.
Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake