Leo July 4, 2018 Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ambaye pia ni Mwenyekiti wa TLP Dr. Augustine Mrema amesema hana mpango wakuhama chama chake bali ataendelea kumuunga mkono akiwa TLP kwa kuwa hakuna rais wa mfano wake hivyo amewataka watanzania kupuuza taarifa zinazoenezwa kuwa ana mpango wa kuhama.
“TLP haijafa msiniache sababu Rais alivyonipenda hajaniambia nitoke TLP, kumbe naweza simamia chama changu na tukafanya kazi na Rais, tumepata rais mzuri hakuna Rais kama Magufuli Tanzania” -Mrema