Leo July 5, 2018 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya ya mafuta kwa mwezi July ambapo bei ya Petroli imeongezeka Shilingi 126 kwa lita huku Dizeli ikiongezeka kwa Shilingi 166.
Kiwango hiki ni kikubwa zaidi kuwahi kutokea kwa mara moja tangu August 2015 ambapo bei ya mafuta iliongezeka kwa Shilingi 92 na kufanya lita moja ya Petroli kuuzwa kwa Shilingi 2290 huku Dizeli ikiuzwa kwa Shilingi 2026 kwa lita.
Kwa jiji la DSM lita moja ya Petroli itauzwa kwa Shilingi 2409 huku Dizeli ikiuzwa Shilingi 2329.
Hali inaonekana kuwa katika mikoa ya Kagera, Geita, Tabora, Songwe, Iringa,Dodoma na Pwani ambapo lita moja ya petroli itauzwa (Sh2,624, Sh2,574, Sh2,563, Sh2,525, Sh2,473, Sh2,467 na Sh2,413) kwa mfuatano.
“Sasa nimekunja NINJA Mbeya mpaka jeshini tutawapata” Kangi Lugola