Leo July 5, 2018 Akiwa mkoani Mbeya Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amelivunja Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na mabaraza yote ya ngazi ya mkoa.
Kangi Lugola amesema hajaridhishwa na utendaji wa baraza katika kukabiliana na ajali za barabarani.
“Kwa mamlaka niliyo nayo kwenye sheria hii ninavunja rasmi Baraza la Usalama Barabarani la Taifa, nakuanzia sasa navunja kamati zote za Usalama Barabarani za Mikoa yote na Wilaya na nitaziunda upya ili kuahakikisha tunaokoa maisha ya wenzetu” Lugola
“Nilikuwa namuuliza mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani nikabaini hajui hata sheria inayoliweka baraza hilo na hata kanuni zake hazijui, hii inaonyesha hatuna baraza,” amesema Lugola.