Leo July 5, 2018 Mbunge wa jimbo la Kyerwa mkoani Kagera Innocent Bilakwate amesema wakulima wa kahawa wanakabiliwa na changamoto katika zao hilo ikiwa ni pamoja na kupigwa, kunyanyaswa na kukosa malipo kwa muda pindi wanapopeleka kahawa yao katika vyama vya msingi, huku akisema kuwa kuna baadhi ya polisi wametumia nafasi hiyo kula Rushwa.
Akimuomba Meneja wa Chama cha Ushirika KDCU kutoa majibu ya malipo ya kahawa katika mkutano wa hadhara amesema kuwa wasipopata ufumbuzi wa zao hilo wataandamana hadi Rais Magufuli apate taarifa ili wasaidiwe.
Kwa upande wake Meneja wa Karagwe District Cooperative Union Limited Kakuru Burchard amesema kuwa mfumo mpya ndo umeleta changamoto lakini anamini wataendelea kuufanyia utafiti maana ni mfumo mzuri kwa wakulima.