Leo July 6, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema alitaka kuchukua uamuzi wa kumfukuza kazi Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mbeya na Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Kagera lakini Happy Birthday yake ndio imewaokoa.
Hata hivyo, Lugola amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuwashusha vyeo Makamanda hao.
Akizungumza na waandishi wa habari, Lugola amesema wakati anaapishwa na Rais alimwambia anachukizwa na matukio ya ajali yanatotokea hasa ya Mbeya.
“Ajali nyingi zinatokea Mbeya ambapo ilinibidi niende kwa Kamati ya Usalama, nilibaini kitu kilichofanya nivunje Mabaraza ya Kamati ya Usalama barabarani,”.
Amesema kuwa alichobaini alitaka kujua kuna wajumbe wangapi lakini walishindwa kujua idadi, wala majina, pia wameshindwa kumpa taarifa ya kile wanachokifanya.
“Hivyo lazima nichukue hatua kali ili kunusuru maisha ya watu kwani Rais amechoka kutuma salamu za rambirambi,”.
Kutokana na hatua hiyo amesema anamuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, awashushe vyeo Makamanda hao kutokana na uzembe.
“Leo nilipanga niwafukuze watu kazi ila bahati nzuri kwao mimi nilizaliwa Ijumaa na kwa vile niliimbiwa wimbo wa Happy Birthday To You….nikaona nisiaribu furaha yangu, hivyo nikawaacha,” amesema.
MAGAZETI LIVE: Umaarufu wa JPM washuka, Hatujamfukuza Nape CCM