Taasisi ya mfanyabiashara na moja kati ya matajiri vijana Afrika Mo Dewji imetoa msaada wa Tsh. 125 Milioni kwa kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ili kusaida kugharamia matibabu ya magonjwa ya saratani kwa watoto wanaopatiwa huduma katika kituo hicho.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Rachel Chengula alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo imekuwa ikitolewa na taasisi kwa kituo hicho.
“Kama upo hai na mwanao anapumua, mshukuru Mungu kuwa ana makusudi na wewe na ana makusudi na mtoto wako. Usikatishwe tamaa na magonjwa, tunaamini kwamba watoto hawa watapona na kurudi nyumbani, watasoma na watalitumikia Taifa letu”>>> Rachel Chengula
“Kama mnavyofahamu Mohammed Dewji amekuwa akifanya kazi na Tumaini la Maisha tangu mwaka 2012 ili kusaidia watoto kupatiwa matibabu, na kupitia taasisi yake tutaendelea kushirikiana ili kusaidia watoto wetu wapatiwe matibabu,”>>> Rachel Chengula
Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake