Leo July 10, 2018 Magari zaidi ya 1700 yamekamatwa na Jeshi la polisi Jijini Arusha kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani katika operesheni iliyoanza July 6, 2018 ambapo zaidi ya Milion 57 zimekusanywa kama tozo kwa makosa hayo kwa siku tatu
Mkuu wa Polisi mkoa wa Arusha Ramadhani Ng’anzi amewaeleza waandishi wa habari kuwa, operesheni hiyo ni endelevu na inalenga kudhibiti ajali mbalimbali zinazotokana na ubovu wa magari.
Amesema katika zoezi hilo jumla ya Madereva 189 walipimwa ulevi na Dereva mmoja alibainika kuwa na kiasi kikubwa cha ulevi mwilini mwake.