Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ambaye yupo Ubelgiji akitibiwa amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho kutumia vizuri fursa ya uchaguzi mdogo wa marudio uliopangwa kufanyika August 12 mwaka huu.
Nanukuu alichoandika Lissu “Hakuna uchaguzi mdogo, kila uchaguzi ni muhimu katika mazingira halisi ya sasa ya kisiasa. Uchaguzi wa marudio wowote ule una kuwa na ugumu wa kipekee, tutafanyiwa na tayari tunafanyiwa kila aina ya fujo na CCM na mawakala wake kwenye Tume ya Uchaguzi na vyombo vya dola”.
Lissu ameendelea kwa kusema “wajibu wetu ni kupambana kwa akili na maarifa ya hali ya juu ili kuzishinda fujo hizo na kushinda chaguzi hizo. Najua ni kazi ngumu, haijawahi kuwa rahisi mahali popote. Hatuna mjomba au shangazi wa kutufanyia kazi hii, au wa kumlilia baadaye tusipoifanya vizuri. Ni jukumu letu pekee”.