Leo July 17, 2018 Moja ya stori ya kuifahamu ni hii Kundi la wanakijiji limewaua karibu mamba 300 kwenye makao ya wanyama katika mkoa wa West Papua nchini Indonesia.
Mauaji hayo yalikuwa ni ya kulipiza kisasi cha kifo cha mwanaume mmoja ambaye aliuawa na mamba katika eneo hilo.
Maafisa na polisi nchini humo wanasema hawakuweza kuzuia mauaji hayo lakini watafungua mashtaka dhidi ya waliohusika.
Kuuawa kwa wanyama wanaolindwa ni kosa nchini Indonesia na adhabu yake inaweza kuwa kifungo jela.
Mwanakijiji huyo aliuawa siku ya Ijumaa asubuhi wakati akitafuta mboga eneo la kuzalia mamba.
Mfanyakazi mmoja alisikia mtu akiomba msaada na alipofika huko aliona mamba akimshambulia mtu.
Baada ya mazishi siku ya Jumapili, wanakijii wenye hasira walielekea eneo la makao ya wanyama wakiwa wamejihami kwa visu, chuma, nyundo na sururu.
Vyombo vya habari vinasema kuwa wanakijiji waliishambulia ofisi kwenye hifadhi ya wanyama na kisha kuwachinja mamba wote 292.