Leo July 19, 2018 tunayo story kuhusu mgunduzi wa madini ya Tanzanite, Mzee Jummane Ngoma ambapo amesafirishwa kwenda nchini India kupatiwa matibabu baada ya kupewa Shilingi Milioni 100 na Rais John Magufuli.
Rais Magufuli alitoa kiasi hicho cha pesa April 2018 wakati alipozindua Ukuta wa Mirerani ambapo alisema ugunduzi wa Mzee Ngoma ndio umeiweka Tanzania katika ramani ya madini hayo.
Kwa mujibu wa mtoto wake, amesema Mzee Ngoma amesafirishwa Jumatatu July 16,2018 kwenda katika hospital ya Apollo nchini India.
Mzee Ngoma amepelekwa nchini humo kwa sababu anasumbuliwa na maradhi ya kupooza.
Inaelezwa kuwa Mzee Ngoma aligundua madini ya Tanzanite miaka 52 iliyopita.