Club ya soka ya AC Milan ya Italia hatimae leo July 20 2018 zimetoka taarifa njema kuhusu club hiyo kutoka kwa chama cha soka Ulaya UEFA, UEFA leo imetangaza rasmi kufuta adhabu ya AC Milan ya kufungiwa kushiriki michuano yoyote ile inayoandaliwa na UEFA baada ya kushinda rufaa yao.
UEFA walitangaza kuifungia AC Milan kwa miaka miwili kushiriki michuano yoyote inayoandaliwa na UEFA kwa sababu ya kukiuka sheria ya usajili ya matumizi ya fedha (Financia Fair Play) ila leo imetoka taarifa mpya kuwa imefutwa adhabu hiyo.
Maamuzi hayo yanakuja ikiwa zimepita siku 27 toka AC Milan itangazwe kupewa adhabu hiyo na UEFA June 27 2018, hivyo kutokana na AC Milan kuwa ilishakata tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Europa League tutawaona wakicheza michuano hiyo msimu wa 2018/19 kama kawaida baada ya adhabu kufutwa na mahakama ya kimichezo CAS baada ya AC Milan kutuma wajumbe kumi na CEO wao Marco Fassone ambao walitoa utetezi huo.
USAJILI WA YONDANI: Manara asema “Mimi ndio msemaji wa SIMBA SC”