Leo July 21, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amezungumza na Waandishi wa Habari kuhusu matamko na maagizo mbalimbali aliyoyatoa tangu aapishwe kushika nafasi hiyo na Rais Magufuli.
Nakusogezea Maagizo 10 aliyoyatoa wakati anaongea na Waandishi wa Habari.
“Nimemuagiza Mkurugenzi wa NIDA afike Ofisini kwangu Dodoma tarehe 25 akiwa na waliopewa tenda ya kuleta mtambo wa kutengeneza vitambulisho vya Taifa kuja kunieleza kwa nini mtambo huo haujaletwa au waje na pesa walizopewa” – Waziri Lugola
“Nimemuagiza Mkurugenzi wa NIDA afike Ofisini kwangu Dodoma tarehe 25 akiwa na waliopewa tenda ya kuleta mtambo wa kutengeneza vitambulisho vya Taifa kuja kunieleza kwa nini mtambo huo haujaletwa au waje na pesa walizopewa” – Waziri Lugola#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/6k2pvt1AWH
— millardayo (@millardayo_) July 21, 2018
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuagiza IGP Sirro kumtafuta mmiliki wa Kampuni ya LUGUMI na kumfikisha ofisini kwake July 31 saa 2 asubuhi.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuagiza IGP Sirro kumtafuta mmiliki wa Kampuni ya LUGUMI na kumfikisha ofisini kwake July 31 saa 2 asubuhi. #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/bJxRJIgtVi
— millardayo (@millardayo_) July 21, 2018
“Nimempa muda IGP Sirro na July 31 nitakutana na wadau wa usafirishaji kuzungumza nao wenye mabasi, wamiliki wa malori pamoja na madereva ili na wao wanipe mtazamo wao juu ya jambo hili la kutembea usiku” Waziri Lugola
“Nimempa muda IGP Sirro na July 31 nitakutana na wadau wa usafirishaji kuzungumza nao wenye mabasi, wamiliki wa malori pamoja na madereva ili na wao wanipe mtazamo wao juu ya jambo hili la kutembea usiku” Waziri Lugola#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/jTOkwaWBVK
— millardayo (@millardayo_) July 21, 2018
“Nilipita kwenye kikosi cha farasi na mbwa ambao wanapewa mafunzo kama askari, kwenye vitabu vya makabidhiano nilikuta dosari ya idadi kubadilika siku moja na nyingine, nilitoa maagizo na IGP ameitisha uchunguzi, tuwape nafasi watupe majibu” Waziri Lugola
“Nilipita kwenye kikosi cha farasi na mbwa ambao wanapewa mafunzo kama askari, kwenye vitabu vya makabidhiano nilikuta dosari ya idadi kubadilika siku moja na nyingine, nilitoa maagizo na IGP ameitisha uchunguzi, tuwape nafasi watupe majibu” Waziri Lugola#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/zeq4Y2wksy
— millardayo (@millardayo_) July 21, 2018
“Hatuwezi kuwa na Jeshi la polisi na wakati huo huo tunakuwa na majambazi yanayotupangia ratiba, yanayotupangia muda wa kufanya kazi, majambazi yanayotuambia huku msije tutafunga mtaa” Waziri Lugola
“Hatuwezi kuwa na Jeshi la polisi na wakati huo huo tunakuwa na majambazi yanayotupangia ratiba, yanayotupangia muda wa kufanya kazi, majambazi yanayotuambia huku msije tutafunga mtaa” Waziri Lugola#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/wg9jB0HO4S
— millardayo (@millardayo_) July 21, 2018
“Katika ziara yangu nilibaini mapungufu kutokana na makabidhiano ya Mbwa na Farasi. Ili kuhakikisha kikosi hiki kinaboreshwa, nimekubalina na IGP Sirro kufanya uchunguzi wa kina na wanipe maelekezo” – Waziri Lugola
“Katika ziara yangu nilibaini mapungufu kutokana na makabidhiano ya Mbwa na Farasi. Ili kuhakikisha kikosi hiki kinaboreshwa, nimekubalina na IGP Sirro kufanya uchunguzi wa kina na wanipe maelekezo” – Waziri Lugola#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/ATlS8cF9ia
— millardayo (@millardayo_) July 21, 2018
“Kuhusu yule askari wa Kikosi cha Zimamoto aliyekuwa anazembea zembea basi tulimchukulia hatua kwa kumvua cheo kimoja kama salamu ili kusiwepo na kauzembe uzembe katika kazi” – Waziri Lugola
“Kuhusu yule askari wa Kikosi cha Zimamoto aliyekuwa anazembea zembea basi tulimchukulia hatua kwa kumvua cheo kimoja kama salamu ili kusiwepo na kauzembe uzembe katika kazi” – Waziri Lugola#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/3dDj4bj7m4
— millardayo (@millardayo_) July 21, 2018
“Bado kumekuwa na baadhi ya askari wanaendelea kulichafua Jeshi la Polisi kwa kuwabambikizia wananchi makosa na kuwalazimisha kutoa rushwa, naomba niwaeleze watanzania, Askari akikikulazimisha umpe rushwa usitoe njoo utoe taarifa kwetu” – Waziri Lugola
“Bado kumekuwa na baadhi ya askari wanaendelea kulichafua Jeshi la Polisi kwa kuwabambikizia wananchi makosa na kuwalazimisha kutoa rushwa, naomba niwaeleze watanzania, Askari akikikulazimisha umpe rushwa usitoe njoo utoe taarifa kwetu” – Waziri Lugola#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/xThnWmKajW
— millardayo (@millardayo_) July 21, 2018
“Ikitokea dereva yoyote amefikishwa Mahakamani bila ya kulazwa mahabusu huyo aliyekufikisha atawajibika yeye” – Waziri Lugola
“Ikitokea dereva yoyote amefikishwa Mahakamani bila ya kulazwa mahabusu huyo aliyekufikisha atawajibika yeye” – Waziri Lugola#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/kpihh2R9Jo
— millardayo (@millardayo_) July 21, 2018
“Nimekubaliana na IGP Simon Sirro kwamba waingie kwa undani sana kufanya uchunguzi wa kujua nini kimetokea kwenye kikosi cha Mbwa na farasi halafu wanipatie ufumbuzi. Hivyo naomba jambo hilo liachwe kwa kuwa lipo katika uchunguzi- Waziri Lugola
“Nimekubaliana na IGP Simon Sirro kwamba waingie kwa undani sana kufanya uchunguzi wa kujua nini kimetokea kwenye kikosi cha Mbwa na farasi halafu wanipatie ufumbuzi. Hivyo naomba jambo hilo liachwe kwa kuwa lipo katika uchunguzi- Waziri Lugola#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/WH0I9EmRIP
— millardayo (@millardayo_) July 21, 2018
TAZAMA LIVE Waziri Kangi Lugola anazungumza na waandishi wa Habari
https://youtu.be/Sq5-o7rA_Jo
Kangi Lugola na IGP Simon Sirro wakutana uso kwa uso