Baada ya taarifa za CHADEMA mkoani Mbeya kutangaza kuwavua uanachama Madiwani wake watatu kwa madai ya makosa ya utovu wa nidhamu baada ya Madiwani hao kukubali mwaliko wa Naibu Spika Dr Tulia Ackson kwenda Bungeni Dodoma pamoja na kushiriki katika baadhi ya shughuli zake, Diwani wa Sisimba Geofrey Kajigili ambaye ni miongoni mwa waliofukuzwa amezungungumza na Waandishi wa habari.
“Hakuna siri Dr Tulia Ackson anafanya maendeleo kwenye jiji letu la Mbeya na nilimsifu kwa hilo, sijapata barua rasmi ya kufukuzwa uanachama na naona wanachelewa wanipe barua leo ili nifanye maamuzi. Mimi nimekuwa nikipigwa vita kwasababu nahimiza maendeleo” – Geofrey Kajigili
Madiwani wa CHADEMA walioalikwa na Dr Tulia wafukuzwa