Club ya Dar es Salaam Young Africans inaonekana kuzidi kuwa katika hali mbaya na hali ya sintofahamu inazidi kutanda ndania ya club hiyo, baada ya awali kuenea kwa taarifa kuwa katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa kajiuzulu.
Leo July 23 2018 kaimu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga nae amaetangaza kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti kwa madai ya kutishiwa na baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni mashabiki na wanachama wa Yanga kuwa wataenda nyumbani kwake kufanya fujo.
Yanga kwa sasa baada ya Clement Sanga kutangaza maamuzi hayo inakuwa haina mwenyekiti wala makamu hiyo inatokana na aliyekuwa mwenyekiti wao Yussuf Manji kujiuzulu miezi kadhaa iliyopita.
USAJILI WA YONDANI: Manara asema “Mimi ndio msemaji wa SIMBA SC”