Moja ya taarifa iliyoripotiwa asubuhi ya leo July 24, 2018 ni pamoja na hii iliyotokea maeneo ya Ubungo Msewe katika Uwanja wa China ambapo watu wanaodaiwa kuwa ni watu wa TANESCO wametoboa matairi ya magari yaliyokuwa yamepaki katika uwanja wa china huku taarifa za awali zikidai ni kwasababu ya nguzo za Umeme mkubwa uliopita katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Msewe amezungumza ambapo yeye anadai kuwa hakupewa taarifa yeyote kuhusu tukio hilo ambapo AyoTV inajitahidi kuwatafuta wahusika kutoka TANESCO ili wazungumzie hilo.