Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney jana usiku alisaini mkataba mpya wa miaka minne wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Mkataba huo umemfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani akiwazidi Leo Messi na Cristiano Ronaldo.
Pamoja na hayo lakini kitu kingine ambacho ulikuwa hufahamu mtu wangu wa nguvu ni kwamba Rooney anayelipwa mshahara wa £300,000 kwa wiki amewazidi mshahara wa viongozi wawili wakubwa duniani Barack Obama na David Cameroon.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron anapata £2,740 kila wiki. Hii ni mara zaidi ya 100 ya mshahara wa Rooney kwa wiki
Na Itamchukua wiki 65 kwa Barack Obama, raisi wa taifa kubwa duniani Marekani, kuweza kutengeneza kiasi anacholipwa Rooney ndani ya siku saba tu – Obama analipwa £240,000 kwa mwaka.