Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof Makame Mbarawa amemtaka Mkurugenzi wa Bandari kuhakikisha meli zote zinazoingia bandarini hapo zinatumia maji ya DAWASCO badala ya watu binafsi yanapakiwa kwenye Maboza.
Prof.Mbarawa ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari bandarini baada ya kuzindua mfumo wa kulipia maji kabla ya kutumia ‘Pre Paid Meter’ utakaofanana na mfumo wa malipo ya umeme ‘LUKU’.
Prof. Mbarawa amesema anatoa agizo hilo kwa sababu maji ya DAWASCO na DAWASA ni salama, hivyo hakuna sababu ya meli kuuziwa maji binafsi yanayopakiwa kwenye maboza.
“Mkurugenzi wa bandari ushirikiane na DAWASCO na DAWASA nataka maji yanayokwenda kwenye meli yawe yanatoka kwao badala ya water Boza,” amesema Mbarawa
LIVE MAGAZETI: Siri nje Jokate kuteuliwa, Mnyukano CCM asilia, Wahamiaji