Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama cha mapinduzi (UVCCM) Kheri James ametolea ufafanuzi kuhusu taarifa iliyosmbazwa mitandaoni ikimtuhumu kutoa maneno ya ubaguzi.
“Kuna upotoshaji umefanyika hivi karibuni, nikiwa mkoani Arusha nilipata nafasi ya kuzungumza na Wananchi wa daraja mbili na nikazungumza mambo mengi sana lakini watu wakachukua sehemu ya maelezo yangu na kuyafanyia siasa. Niliyoyasema mwanzo na mwisho watu hawakuyajua lakini maneno ya katikati yakatumika kwamba tunahimiza ubaguzi” –Kheri James
Agizo moja la Waziri Mbarawa kwa Uongozi wa Bandari ya DSM