Najua ukisikia Urusi kwa sasa utakuwa unakumbuka fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Humo na kumalizika kwa Ufaransa kuwa mabingwa, najua kuna watanzania ambao walipata nafasi ya kwenda Urusi kwa ajili ya kuangalia michuano hiyo lakini hii inawezekana ukawa huijui.
Urusi ni moja kati ya nchi kubwa na ina idadi ndogo ya watu ukilinganisha na ukubwa wake, Urusi ina jumla ya watu milioni 146 lakini nimeipata exclusive kutoka Urusi kuwa raia wake hawapendi kuzaa yaani kupata watoto.
Kiasi cha serikali ya nchi hiyo kuanzisha sheria kuwa ukizaa mtoto wa pili kwa wale raia wa Urusi utalipwa dola elfu 14 na mtoto kulipiwa gharama zote za afya na shule kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu hiyo ukizaa mtoto wa pili na kuendelea kila ukizaa unalipwa dola elfu 14.
“Ninapuuza upotoshaji uliofanyika kwenye kauli yangu” –Kheri James