Club ya Dar es Salaam Young Africans licha ya kuondolewa katika michuano ya Kombe la shirikisho Afrika ikiwa na michezo miwili mkononi ya kukamilisha ratiba, leo imecheza mchezo wake mmoja wa kukamilisha ratiba dhidi ya USM Alger.
Yanga imecheza game yake ya tano ya hatua ya makundi ya michuano ya CAF uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ikiwa ni game yake ya tano ya Kundi D, hiyo ni baada ya kutopata matokeo chanya katika mechi zake nne za mwanzo.
Kwa mara ya kwanza baada ya mechi nne Yanga leo ndio imefanikiwa kuvuna point tatu, baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya Yanga yakifungwa na Deus Kaseke dakika ya 43 na Heritier Makambo dakika ya 47, wakati goli la USM Alger lilifungwa na Abdulrahman Meziane dakika ya 52.
Ushindi huo ni wa kwanza kwa Yanga toka mwenyekiti wao Yussuf Manji aonekane leo kwa mara ya kwanza uwanjani na kuwapa hamasa wachezaji, Manji alijiuzulu nafasi hiyo na baadae wapenzi na wanachama walimuomba arudi kuisaidia timu yao inayoaminika kuwa duni kiuchumi kwa sasa.
Manji aibuka Yanga leo, asema ‘hakuna zawadi kubwa kama……….?’ (+video)