Leo August 21, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Makosa Jinai nchini (DCI) Robert Boaz kumkamata aliekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu kabla ya saa 12 jioni leo.
Pia Waziri Lugola ameagiza kukamatwa kwa wamiliki wa kampuni tatu zinazodaiwa kuhusika katika mradi wa vitambulisho vya taifa, Gotham’s International Limited, Gwiholoto Impex Ltd na Aste Insurance wanaodaiwa kufanya udanganyifu na kushindwa kurejesha fedha walizotumia kinyume na utaratibu.
Akizungumza na waandishi wa habari Lugola ameagiza kukamatwa watumishi wote wa NIDA ambao wanatuhumiwa katika ubadhirifu wa fedha za umma wakishirikina na kampuni hizo.