Leo August 23, 2018 RC Mbeya, Albert Chalamila, ametangza vita na wafanyabiashara wa Dawa za kulevya akiahidi kuwashughulikia na hakikisha biashara hiyo haramu inakoma ili kuwaokoa vijana.
Chalamila ametangaza vita hiyo akizungumza na waathirika wa dawa hizo ambao wameacha kuzitumia na kujiunga na tiba ya Methadol katika Rufaa ya Mbeya.
“Haiwezekani watu wananunua magari ya bei, wanajenga maghorofa kutokana na kuua vijana wetu, sasa natangaza vita na wauza dawa za kulevya katika mkoa huu, nawahakikishia kuwa vita hii mtashuhudia wenyewe,” amesema Chalamila
MACHOZI: Rais Magufuli akimuongoza Mama yake kuaga Mwili wa Monica